1. Songs

74. Niambie, Ee Mlinzi

Nyimbo za Kristo

Verse 1

Niambie, Ee Mlinzi, Umepambazuka Je!

Utukufu Wa Zayuni; Pana Dalili Zake?

Msafiri Uondoke, Utazame Mbinguni,

Kiunoni Ujifunge, Ni Kucha, Alifajiri.

Verse 1

Mlinzi, Inamulika Nuru Njiani Mwako,

Dalili Ya Kuja Kwake, Kwamba Siku Karibu;

Panda Itakapolia Itawaamsha Wafu,

Watakatifu Wa Mungu, Kuwapa Kutokufa.

Verse 2

Mlinzi, Ione Nuru Ya Mwaka Wa Sabato;

Sauti Zina Tangaza Ufalme Ni Karibu:

Msafiri Ninaona Mlima Wa Zayuini,

Mji Wa Yerusalemu Nayo Fahari Yake.

Verse 3

Kwenye Mji Wa Dhahabu Anaketi Mfalme

Katika Kiti Kizuri: Huku Ana Tawala.

Pana Amani Po Pote, Mashamba Husitawi;

Na Ardhi Ina Rutuba; Mito Ni Mitulivu.

Verse 4

Mlinzi, Twakaribia Nchi Iliyo Nzuri;

Twende Mbele, Tufurahi, Nchi Inachangamka.

Sikieni Kuna Wimbo Wa Waliookoka;

Kaza Mwendo, Ujiunge Na Kundi Kubwa Hili.

Present this song in WorshipOne →Ready-made slides, chord transposition and mobile remote control.
Share
Transpose in WorshipOneEdit in WorshipOne

More Swahili songs